MABAO matatu aliyofunga
mshambuliaji wa kimataifa Uholanzi Robin van Persie katika ushindi wa
mabao 8-1 dhidi ya Hungary wa mechi za kufuzu michuano ya Kombe la Dunia
umemfanya kuwa mshambuliaji aliyefunga mabao mengi zaidi katika nchi
yake. Van Persie
alifikisha mabao 41 katika mechi 80 alizocheza katika timu ya taifa na
kuizidi rekodi iliyowekwa na Patrik Kluivert katika mechi hiyo
iliyopigwa jana usiku. Van
Persie ambaye anacheza katika klabu ya Manchester United alifunga bao
la kuongoza kwa timu yake katika dakika ya 15 kabla ya kuifikia rekodi
hiyo ya mabao ya taifa kwa kufunga bao lingine kabla ya mapumziko. Nyota
huyo aliongeza bao lingine katika dakika 52 na kufanya idadi ya mabao
aliyoifungia timu ya taifa kufikia 41 na kumpita Kluivert aliyekuwa
akishikilia rekodi hiyo kwa kufunga mabao 40.
Home »
michezo ulaya
» VAN PERSIE AWEKA REKODI UHOLANZI.
VAN PERSIE AWEKA REKODI UHOLANZI.
Written By Unknown on Saturday, 12 October 2013 | Saturday, October 12, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!