MENEJA wa klabu ya
Arsenal, Arsene Wenger ameunga mkono madai ya kiungo Jack Wilshere kuwa
Waingereza pekee ndio wanapaswa kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo. Mshambuliaji
wa Manchester United mzaliwa wa Ubelgiji Adnan Januzaj anaweza
kuitumikia timu ya taifa ya nchi hiyo kama akichukua uraia. Akiulizwa
kuhusiana na suala hilo Wilshere mwenye umri wa miaka 21 amesema kama
mtu ameishi Uingereza kwa miaka mitano haimfanyi kuwa mwingereza. Kauli ya nyota huyo ilizua mjadala mkubwa lakini Wenger ameonyesha kukubaliana na maneno ya kiungo wake huyo. Hata
hivyo Wilshere ambaye amecheza mechi 10 katika timu ya taifa ya
Uingereza amesema kauli yake haijamlenga Januzaj ambaye meneja wa
Uingereza Roy Hodgson alithibitisha kufuatilia nyendo zake.
Home »
michezo ulaya
» WENGER AUNGA MKONO KAULI YA WILSHERE.
WENGER AUNGA MKONO KAULI YA WILSHERE.
Written By Unknown on Friday, 11 October 2013 | Friday, October 11, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!