STRAIKA wa Simba, Mrundi Amisi Tambwe, amewaambia Yanga kuwa wanamtafuta ubaya na atawakomesha Jumapili, timu hizo zitakapoumana Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Tambwe, ambaye ni kinara wa mabao wa Ligi Kuu
Tanzania Bara msimu huu hadi sasa, anaongoza kwa kutikisa nyavu mara
nane na hiyo Jumapili atakuwa na kazi ya kuinyamanzisha Yanga ambayo
viongozi wake wametoa ahadi nzito za kushinda.
Akizungumza na vyombo vya Habari, Tambwe alisema: “Yanga
itambue kuwa sisi ndiyo tunaongoza ligi na tunawazidi kwa kila kitu. Kwa
upande wangu niko vizuri, ninamwomba Mungu anipe afya njema hadi
Jumapili ili niwafunge mabao na kuwafunga midomo yao.
“Wanapaswa kufahamu kuwa mpira hauchezwi kwa
maneno ila ni dakika 90 za uwanjani, kama wakishinda ndiyo wazungumze na
sisi tukifungwa tutanyamaza.

Kuhusiana na madai kuwa mara nyingi mechi hiyo
huwa pia na mambo ya kishirikina, Tambwe mwenye mabao nane mpaka sasa
alisema: “Siogopi kitu ushirikina, kwangu uchawi wa soka ni mazoezi na
maandalizi tu.”
Akiizungumzia safu ya ulinzi ya Yanga yenye akina
Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, alisema: “Kama
nilivyosema simwogopi yeyote.”
Kwa upande wao mabeki hao kwa nyakati tofauti wameahidi kumdhibiti Tambwe wakisema hatafanikiwa kuwapita.
Naye Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibadeni
‘Mputa’ alisema: “Nipo kambini kwa ajili ya kuandaa timu yangu iweze
kishinda na sijui ya wengine.”
Beki wa kati wa Simba, Mrundi Kaze Gilbert,
ametamka kuwa, safu yao ya ulinzi ipo kamili na mechi dhidi ya Yanga
watahakikisha wanakaba kila kitu hadi kivuli.

“Mechi hiyo ni ngumu, lakini safu yetu ni imara kuhakikisha hatutoi nafasi yoyote.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!