Mahakama
kuu jijini Nairobi nchini Kenya imeahirisha kesi inayowakabili
watuhumiwa wanne raia wa Somalia kwa kuhusika kwao kwenye shambulio la
kigaidi la Westgate mwezi mmoja uliopita.
Watuhumiwa wanne wa
kupanga njama za shambulio la Westgate walipandishwa kizimbani kwenye
mahakama ya Milimani kusomewa mashtaka yanayowakabili ambapo kesi yao
iliahirishwa hadi tarehe 15 mwezi January mwakani.
Majaji wanaosikiliza kesi hiyo wamesema kuwa kesi yao itaanza kusikilizwa rasmi mwakani mwezi January wakati huu ambapo maofisa usalama wakiendelea kukusanya ushahidi kuwahusisha na tukio hilo
Mahakama imeongeza kuwa watuhumiwa hao wanne watajua hatma yao hapo mwakani iwapo watapatiwa dhamana au la kulinga na makosa ambayo yako mbele yao ya kuhusika na kuwasaidia watu waliotekeleza shambulio la Westgate.
Watuhumiwa hao raia wa Somalia ni pamoja na Liban Abdulah, Hussein Hassan na Adan Mohamed ambao wote kwa pamoja hawakutakiwa kujibu chochote.
Kwa mujibu wa mwandishi wetu James Shimanyula aliyekuwepo mahakamani upande wa mashtaka ulita watuhumiwa hao wasipatiwe dhaman kutokana na makosa yanayowakabili kuwa ni yaugaidi yasiyohitaji dhamana.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!