STRAIKA wa Simba, Amissi Tambwe alitarajiwa kuondoka jana Ijumaa saa 12:40 jioni kwa Ndege ya Rwanda Air ambayo ingemleta hapa nchini kwa ajili ya mapumziko.
Hata hivyo licha ya kuwa katika mapumziko, kuanzia
Novemba 18 atarudi uwanjani akijichanganya na kikosi cha Vital’O ya
Burundi kujiweka sawa ili kwenda sambamba na mastraika wanaokuja kwa
kasi kama Hamis Kiiza wa Yanga.
Tambwe anaongoza ufungaji katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao 10 huku Kiza akifuata akiwa na mabao manane.
Mchezaji huyo alisema angependa kujiunga na timu
ya Taifa ya Burundi kwa ajili ya michuano ya Chalenji itakayochezwa
mwezi huu nchini Kenya lakini amechoka na kwa ugumu wa ligi ya Tanzania itamhitaji apumzike ili kurejea kwa kishindo Januari.
Katika hatua nyingine, Tambwe amewashangaa wengi
wanaomuita Didier Kavumbagu wa Yanga mshambuliaji wakati ni kiungo.
“Lakini kwa soka ni kitu cha kawaida, mchezaji kucheza sehemu fulani
kwenye timu ya Taifa na kwenye klabu akapangwa tofauti ingawa kwa mimi
namjua Kavumbagu huwa ni kiungo tena anajua kuchezesha mpira lakini
nashangaa kuona Yanga wakimtumia kama mshambuliaji.
“Timu ya Taifa ya Burundi huwa anatumiwa kama
kiungo mchezeshaji na huwa anajua kutoa pasi nzuri kwa washambuliaji
wanaokuwepo,”alisema Tambwe huku akisema kuwa atashawishika kujiunga na
timu ya Taifa kama ataletewa mchezeshaji kama Kavumbagu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!