Akili ya wasanii wanaojielewa siku zote huwa iko mzigoni haijalishi msanii yuko baa, hotelini, maskani,kanisani, back stage anasubiri kupiga show, jela na sehemu yoyote ile .
Kwa sisi waandishi wa habari sifa kubwa ya mwandishi ni kuwa na kitu kinaitwa ‘Nose for News’, sasa msanii anatakiwa kuwa na ‘Nose for Hits’.
Mkusanyiko wa utani, ushikaji na ubunifu ni vitu ambavyo viko nyuma ya story ya hit song iliyochukua tuzo za BET mwaka huu , ‘Fu***n Problem’ ya A$AP Rocky akiwa amewashirikisha 2 Chainz, Drake na Kendrick Lamar.
Story iko hivi, Drake alikuwa studio anagongagonga mdundo bila kuambiwa na mtu yeyote, na humo studio alikuwemo A$AP Rocky akiandika wimbo wake ambao alikuwa bado hajaupa jina na alijikuta tu anapata mzuka zaidi wa kuuandika kwa kutumia mdundo uliokuwa unagongwa na Drake.
Mwisho akamwambia Drake kiutani kuwa mdundo wake ni kama umekaa kwenye ngoma anayoandika yeye muda huo, wakiwa bado wanalonga kishikaji huku A$AP Rocky akiwa anajaribu mistari yake kwenye huo mdundo, ghafla akaingia 2 Chainz studio akiwa na mishemishe zake.
Kiutani, 2 Chainz bila kujua kilichokuwa kinaendelea mle ndani aliingia akiwa anaimba ‘kitu’, lakini kabla hajatulia A$AP Rocky akamwambia hicho anachokiimba kitafaa kuwa chorus ya wimbo wake ambao mdundo wake ndio huo ameugusa Drake.
Mwisho wa siku idea hiyo ya mdundo wa Drake ikawekwa sawa zaidi na producer Noah ‘40’ Shebib. Mzigo ukakamilishwa akaongezwa King of New York Kendrick Lamar.
Na tangu wimbo uachiwe October 24, 2012 ulimpeleka A$AP Rocky juu ambapo kwa mara ya kwanza wimbo wake uliingia kwenye chart za UK, lakini pia ulishika nafasi ya 8 kwenye Billiboard Hot 100.
Lil Wayne ameutumia mdundo wa ngoma hiyo kwenye mixtape yake Dedication 5, lakini wakali wengi wameshafanya mitindo huru kwa kuirudia idea ya ngoma hiyo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!