Si rahisi hata kidogo msanii kupewa heshima ya barabara kubadilishwa
jina na kuitwa jina lake, lakini hiyo iliwezekana kwa Justin Bieber
mwaka 2011. Ni baada ya msichana mwenye miaka 11 kushinda shindano la
Facebook la kuwa meya kwa siku moja mwaka 2011.
Badala ya kujikita katika masuala mazito na yenye tija kwa umma kama vile ukosefu wa ajira, uhalifu na mambo mengine, msichana huyo, Caroline Gonzale, aliamua kubadilisha jina la barabara iliyopo kwenye mji mdogo wa Forney, Texas, na kuipa jina la msanii ampendaye, Justin Bieber.
Caroline aliiambia E! Online sababu za kuiita barabara hiyo jina la Justin: Napenda muziki wake na nampenda. Na nikafikiria kwanini tusiwe na mtaa kwenye mji wetu wenye jina la msanii nimpendaye ?”
Hata hivyo mzuka wa Bieber uliondoka mapema baada ya wezi kuuiba alama ya barabara hiyo siku mbili tu baada ya kuwekwa.
Alama hiyo imewekwa tena na bado barabara hiyo ina jina la Justin Bieber hadi leo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!