Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » AZIMIO DHIDI YA UJASUSI LAPASISHWA NA UN

AZIMIO DHIDI YA UJASUSI LAPASISHWA NA UN

Written By Unknown on Thursday, 19 December 2013 | Thursday, December 19, 2013

Katika kile kinachoonekana ni ukosoaji wa kimataifa kwa ujasusi wa Marekani, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepetisha kwa sauti azimio linalolenga kulinda haki ya faragha dhidi ya ujasusi unakiuka sheria.
Ujerumani na Brazil ziliwasilisha azimio hilo baada ya kubainika kuwa mfanyakazi wa zamani wa Wakala wa Usalama wa Taifa wa Marekani (NSA) Edward Snowden kuwa shirika hilo la kijasusi lilikuwa likisikiliza kwa siri mazungumzo ya viongozi wa kigeni akiwemo rais Dilma Roussef wa Brazil na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Azimio hilo linazitaka nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa kudhamini haki ya faragha ya watumizi wa intaneti na shuhula nyinginezo za mawasiliano ya elektroniki. Azimio hilo limeelezea wasi wasi wake kuwa ujasusi kama uliofanya na Mareknai ni chanzo cha ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu. Rais wa Brazil alivunja mpango wake wa kuenda Marekani baad aya kubainika kuwa mashirika ya kijasusi ya Marekani yalikuwa yakisikiliza kwa siri mazungumzo yake ya simu.  Ikumbukwa kuwa Snowden alifichua ujasusi mkubwa unaofanywa na Marekani kupitia programu ya kijasusi ya PRISM katika kona zote za dunia.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi