Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BAADA YA MAPAMBANO MAKALI NA WAASI SASA JESHI LA NCHINI SUDAN KUSINI LATANGAZA KUUDHIBITI TENA MJI WA BOR

BAADA YA MAPAMBANO MAKALI NA WAASI SASA JESHI LA NCHINI SUDAN KUSINI LATANGAZA KUUDHIBITI TENA MJI WA BOR

Written By Unknown on Wednesday, 25 December 2013 | Wednesday, December 25, 2013

Jeshi la Sudani Kusini limetangaza kwamba limefaulu kuurejesha mikononi mwa serikali mji wa Bor uliokuwa unadhibitiwa na wapiganaiji waasi wanaomtii makamo wa rais wa zamani Riek Mashar. mapiganao makali yameshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini humo, huku Umoja wa Mataifa ukiidhinisha azimia la kuongeza wanajeshi zaidi wa kulinda amani nchini humo.

Mapigano haya yanaendelea licha ya kila pande kuwa tayari kuketi kwenye meza ya mazungumzo. Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini, Riek Machar amesema ataweza tu kuzungumza na rais Salva Kirr hadi pale atakapowaachilia huru wanasiasa wanaouzuiliwa.
Kauli hiyo ya Riek Mashar inakuja wakati, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kauli moja limepitisha azimio la kuongezwa kwa majeshi zaidi ya kulinda amani nchini Sudan Kusini.
Hii inaaminisha kuwa idadi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa huko Sudani Kusini itakuwa ni zaidi ya wanajeshi elfu kumi na mbili katika taifa hilo changa linalopitia kipindi kigumu cha machafuko kati ya wanajeshi wa serikali na wale wanaomuunga mkono aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa maelfu ya watu wamepoteza maisha kutokana na mzozo huo na siku ya Jumanne wamegundua uwepo wa makaburi ya pamoja mjini Juba na Bentiu.
Ban Ki-Moon amesma licha ya kuongezwa kwa wanajeshi hao haimaanishi kwamba watalinda usalama wa raia wote nchini humo.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu 80,000 wamekimbia makwao na wanahifadhiwa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Francis M Deng balozi wa Sudan Kusini katika Umoja wa Mataifa, amesema wanaishukuru Jumuiya ya Kimataifa kwa kuendelea kuisaidia Sudan Kusini ili iwe na amani, na kuiomba isichoke.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi