Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BAADA YA MITINDO YA NYWELE NA NGUO ZA AINA YA KIDOTI SASA JOKATE AJA NA CLUB

BAADA YA MITINDO YA NYWELE NA NGUO ZA AINA YA KIDOTI SASA JOKATE AJA NA CLUB

Written By Unknown on Thursday, 19 December 2013 | Thursday, December 19, 2013

BAADA ya kutamba na mitindo ya nywele na nguo aina ya Kidoti, mrembo, Jokate Mwegelo ameanzisha klabu yake aliyoipa jina la Kidoti Club.
Akizungumza katika uzinduzi wa klabu hiyo jana Jumatano, Jokate alisema Kidoti ni tofauti na klabu nyingine kwani atakuwa anajihusisha na mambo mbalimbali katika jamii hususani urembo na mitindo.
Jokate alisema kupitia klabu yake atakuwa anatoa ushauri pamoja na taarifa za muziki, filamu, wasanii na nyinginezo kwa ajili ya rika tofauti.
Jokate, Miss Tanzania namba mbili wa mwka 2006, alisema ili uwe mwanachama unatakiwa kutuma neno kidoti kwenda namba 15678 na kuanza kupata taarifa kutoka kwake. “Ni mfumo wa kisasa wa kutoa taarifa mbali mbali kwa jamii, hata Beyonce amefanya hivyo na kwa sasa hakuna mtu anayeingia katika shoo zake bila kuwa mwanachama wa klabu yake, mimi pia naelekea huko, nitaweka taarifa zangu na ili kupata lazima uwe mwanachama,” alisema ambaye pia ni mbunifu wa mavazi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi