Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » BAADA YA WENGINE WAKIJIANDALIA KUUMALIZA MWAKA 2013 VIZURI ILA NISHA WAMMALIZIKIA VIBAYA

BAADA YA WENGINE WAKIJIANDALIA KUUMALIZA MWAKA 2013 VIZURI ILA NISHA WAMMALIZIKIA VIBAYA

Written By Unknown on Monday, 23 December 2013 | Monday, December 23, 2013

Maskini! Staa wa sinema za Kitanzania,Salma Jabu ‘Nisha’ anateseka baada ya kupata gonjwa la ajabu linalomsababishia maumivu makali.Akizungumza rafiki yake ambaye pia ni msanii mwenzake, Happy John ‘Nyatawe’ alisema Nisha alianza kulalamika kwamba anasikia vitu vikimtembea mwilini na maumivu makali ya kichwa kinachomuuma mfululizo.
“Alianza kulalamika kuumwa kama mchezo lakini siku zinavyozidi kusonga ndivyo hali yake inavyozidi kuwa mbaya, hata hatuelewi ni nini,” alisema Nyatawe.

Paparazi wetu alifanikiwa kuzungumza na Nisha akiwa nyumbani kwake huku akilishwa chakula kama mtoto ambapo alisema anasikia maumivu makali ya kichwa na tayari ameshaenda hospitali akapewa dawa lakini ugonjwa unaomsumbua haukujulikana.
“Kichwa kinaniuma sana na vitu vinanitembea mwilini sijielewi kabisa, muda mwingine ninakandwa na maji ya baridi kutokana na maumivu makali, nimeenda hospitali nimepima kila kitu lakini ugonjwa hauonekani,” alisema Nisha akitokwa machozi kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia.
Wakati paparazi wetu akiendelea na mazungumzo hayo alimshuhudia Nisha akiweweseka kama mtu aliyechanganyikiwa.

Baadhi ya wasanii ambao hawakutaka kutajwa walisema kutokana na hali aliyonayo Nisha inawezekana kuna mkono wa mtu kwani wasanii wamezidi kwa kulogana hivyo anatakiwa kuombewa kwa Mola kwani hali ya afya yake si shwari.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi