Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BOB JUNIOR AJIANDA KUIGHARAMIA VYAKUTOSHA VIDEO YA TRACK YAKE MPYA YA BASHASHA

BOB JUNIOR AJIANDA KUIGHARAMIA VYAKUTOSHA VIDEO YA TRACK YAKE MPYA YA BASHASHA

Written By Unknown on Thursday, 19 December 2013 | Thursday, December 19, 2013

Wasanii wa nchini Tanzania wameendelea kuwekeza vya kutosha kwenye video za nyimbo zao ili ziweze kupata nafasi ya kuchezwa kwenye vituo vikubwa vya televisheni duniani.
Rais wa Masharobaro kama anavyojiita, Bob Junior amesema kuwa anatarajia kutumia zaidi ya shilingi za kitanzania million 16 kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake ‘Bashasha’ aliomshirikisha Vanessa Mdee, video ambayo itafanywa na Ogopa Videoz ya Kenya  .
“Kiukweli katika ngoma ambazo zimehit haraka sana kuliko ngoma zangu zote bila audio na video hii ni ya kwanza ukilinganisha na nyimbo zangu za kwanza, kwenye ringtone za watu imewekwa na watu wengi, pia kwenye facebook, instagram na watsup unakuta watu wananitumia verse za nyimbo yangu. Na ndio maana hata imenichanganya kufanya video kubwa sana, nimeandaa karibu dola 10,000 (zaidi ya million 16 za Tanzania) kufanya video nzuri.” Bob Junior amesema.
Mwimbaji huyo alieleza sababu za kuipeleka hiyo Million 16 nchini Kenya huku akiyaacha makampuni ya nchini mwao.
“Muda mwingi sana nilikuwa na dream ya kufanya kazi na Ogopa na napenda jinsi wanavyoshoot, quality yao, na wanatumia camera kubwa ya RED. So, I wish to make something big unajua, sio kila siku matawi yangu yanabakia hapa. Na kwa upande mwingine Ogopa wana channel ndefu, wana tuzo nyingi wamechukua hadi South Africa, anapigwa TRACE, anapigwa kwenye TV nyingi za kimataifa. Kampuni ambazo ziko hapa hawawezi kumfikia Ogopa kwa kweli, yuko more advanced.”
Amesema video hiyo itashutiwa nchini Tanzania na Kenya, na kwamba itazinduliwa December 24 mwaka huu huko Zanzibar, na December 29 Dar es Salaam.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi