Ufaransa imeelezea msimamo wake wa kutoelemea upande wowote katika mzozo
wa Jamhuri ya Afrika kati,msimamo ambao wataalam wanahisi ni shida
kuutekeleza katika wakati ambapo mshirika wake wa karibu Chad,haiufuati.
Serikali ya Chad imekanusha kuhusika na mashambulio hayo.
Mashambulio yameripotiwa pia kati ya wanajeshi wa Chad na wale wa Burundi wanaotumikia kikosi cha MISCA. Wanajeshi wa Chad wanasemekana waliwarushia guruneti wanajeshi wa Burundi walipokuwa wakiwapokonya silaha waasi wa zamani wa Seleka.
"Wanajeshi wa Chad wameondoka pamoja na waasi wote sita wa Seleka na kuanza kufyetua risasi kila upande,wamerejea baadae na kuanza kushambulia vituo vyetu" mkuu wa kikosi cha Burundi Luteni kanali Pontien Hakizimana amesema.
Ufaransa Yasema Haielemei Upande Wowote
Duru za kijeshi zinasema uhusiano kati ya wanajeshi wa Chad na wale wa Burundi katika kikosi cha MISCA,umezorota tangu wanajeshi wa Chad walipowekwa nje ya mji mkuu na wanajeshi wa Burundi kupewa jukumu la kulinda amani mjini Bangui.
Ikionyesha hamu ya kutaka kuendelea kuwa na mshirika wake katika eneo hilo,anayewasaidia pia katika vita dhidi ya ugaidi nchini Mali,Ufaransa imeelezea umuhimu wa kujulikana ukweli kuhusu kuuliwa mwanaharakati huyo.Ufaransa imeelezea pia "imani yake kamili kwa rais Idriss Deby wa Chad,mshirika mkubwa aliyetuma wanajeshi 850 katika kikosi cha kulinda amani cha MISCA katika Jamhuri ya Afrika kati.
Katika wakati ambapo wanajeshi wa Ufaransa wanalaumiwa na waandamanaji wanaowaunga mkono Seleka kufanya mapendeleo rais Francois Hollande amesisitiza kuhusu misingi ya kutoelemea upande wowote wanajeshi wa Ufaransa.
Maandamano dhidi ya Opereshini Sangaris
Ahmed Adam akisimama mbele ya msikiti mjini Bangui
Licha ya ahadi hizo maandamano yameripoitiwa tena dhidi ya
opereshini za wanajeshi wa Ufaransa Sangaris katika Jamhuri ya Afrika
Kati.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!