Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » HUYU NDO MWANAMUZIKI WA BURUNDI ALIE TUMIA POMBE KUPITA KIASI HADI KUONGEA MAMBO YA AJABU JUKWANI AKIWA KWENYE SHOW

HUYU NDO MWANAMUZIKI WA BURUNDI ALIE TUMIA POMBE KUPITA KIASI HADI KUONGEA MAMBO YA AJABU JUKWANI AKIWA KWENYE SHOW

Written By Unknown on Saturday, 28 December 2013 | Saturday, December 28, 2013

Kitendo cha ajabu alicho kifanya star wa Bajou namzungumzia Mugani Desire alimaarufu kama Burundiano jana kwenye viwanja vya Tempete pale Quartier Asiatique mwanahabari Mh Ismail NIYONKURU amekilaani nakusema kuwa ni kitendo cha utovu wa nidhamu kwa mwanamuziki kama huyo ambae anajiita kuwa ni star wa Burundi na mwenye tabia za kupaswa kuigwa.Hayo yamezungumzwa na Mwanahabari Mh Ismail NIYONKURU kwenye mahojiano na mtandao huyu mapema alfajiri ya leo baada ya kuwa mwanahabari huyo alitembelea pale kwenye maonyesho ya biashara ambayo yametinga kambi kwenye viwanja hivyo vya Tempete na jana alikua amealikwa mwanamuziki huyo kwenda kuburudisha wateja wanao kuja kushuhudia maonesho hayo ya biashara kama njia moja wapo yakuvuta wateja.
Kwenye mida ya saa tatu kasoro za usiku mwanahabari huyo anasema alipo kuwa anatokea kwa mtu wake wa nguvu ambae ni Brother wake goal kipa wa timu ya taifa Arakaza Marc Arthur ilimbidi ashukie usafiri wake pale kwenye viwanja hivyo vya Tempete ili kushuhudia show ya mwanamuziki huyo,udogo wa watu ulio kuwepo hapo ulikuwa ukigubikwa na wanawake wenye umri mdogo yani ma binti na wenye rangi za kiarabu walikuwa kibao,huku star huyo akitowa burudani kidogo kidogo raia na udogo wao walionekana kumshangilia star huyo.
Ila star huyo alionekana kuwa kwenye mazingira ambayo sio ya kawaida yake baada yakuonekana na kusikika akizungumza mambo ambayo si kawaida yake yeye kuwa anayazungumza akiwa jukwani,alionekana zaidi akizisahau hata bahazi ya nyimbo zake za hapo mwanzo kuzirudilia na vile alikua akipiga playback.
Muda vile ulivyo kuwa ukisogea mbele na ndo vile star huyo alionekana kudhihirisha kama alikuwa amelewa zaidi ya kipimo muda mchache baadae sauti za baadhi ya raia zilianza kusikika huku zikisema"amesha lewa....we haumuoni vile alivyo".
Mwanahabari Mh Ismail NIYONKURU alipigwa na butwa kwa kumuona star huyo analewa hadi kila mtu wote kuvishuhudia,mwanahabari huyo ameongeza nakusema kuwa hakuna kilicho muuma roho zaidi na kuwa kama anamvuja nguvu ni pale star huyu alipo sema hazarani kuwa anakiwi...
"Nina kiwi cha un million...kweli nina kiwi cha un milion...nyie mko mnakunywa ila mimi siko nakunywa...."alisikika akiongea huku akiwa kwenye jukwaa.
Baadae muda mchache dada umoja mwenye asili ya kiarabu alionesha moyo wa upendo kwa mwanamuziki huyo nakwenda kumnunulia maji aina ya Sangwe lakini shabaha ya Fizzo haikuwa maji na wala yale ya kuwa eti anasikia kiwi hakusema kwa maana halisi ila ilitokana na kuwa alikuwa ametumia pombe kupita kiasi hadi kuongea ambayo hayapaswi kuzungumzwa ukiwa jukwani tena kwa mwanamuziki kama huyo ambae uma wa wa warundi unamtizama yeye.
Fizzo alionekana kumshobokea dada huyo wa kiarabu huku akimuomba ampe namba yake ya simu huku dada huyo wa kiarabu akitaka kuondoka yeye anakuwa anamrudisha nakumwambia abaki aongee na yeye.Dada huyo aibu kumzidi alimbidi aondoke huku dada huyo akitupia kicheko.
Hali hiyo yote ilieleweka kuwa ilikuwa ni pombe alizo kunywa mwanamuziki huyo ambazo zilimpita kipimo.
Baadae muda mchache kulionekana kunaletwa chupa za Beer jukwaani beer ambazyo haikutambulika na wale waliokuwa mbali na jukwa kama ni beer aina gani lakini sauti ya Fizzo ilisikika ikisema hivi"hivi hizi Heinken nne ntazimaliza kweli sizitaniuwa..."
Bila ya aibu mwanamuziki huyo alianza kuzinywa moja kunyingine kidogo kidogo huku akiwa jukwani jambo ambalo raia walionekana kuchukizwa na kitendo hicho cha utovu  wa nidhamu.
Ila hali yote hiyo ilikuwa ikisababishwa na pombe nyingi alizokuwa amekunywa mwanamuziki huyo,muda mchache baadae alisikika akisema hivi"Msiende kunisema eti Fizzo alikunywa pombe jukwaani....uuuuuuhhhh uuuuuhhhh nawaomba huyu ni mwaka mpya......msinisemeeee jamani...."alisikika akisema 
Baadae mwanahabari Mh Ismail NIYONKURU alijaribu kutaka kuongea na Fizzo alipo maliza ku parfom ndipo alijionea vizuri kuwa mwanamuziki huyo alikuwa amelewa kupita kiasi huku mwanamuziki huyo alipo mpiga jicho mwanahabari Mh Ismail Niyonkuru alionekana kumjia mkali mwanahabari huyo nakuanza kumkumbusha baadhi ya taarrifa alizo zitangaza mtangazaji huyo kwenye kipindi chake na zikawa zilimkera mwanamuziki huyo nakusema kuwa hawezi kuongea na yeye.
Mwanamuziki huyo alionekana kukumbusha ile habari ambayo ilikuwa kama siri imefichwa nakufichuliwa na mwanahabari huyo majuma kadha yaliyo pita yakuwa alicopy na ku past beat ya Track ya "Track sound"yakwake May D  wa Nigeria na kuitumia kwenye Track "Daima" yake na Samanta.
Hadi sasa inasemekana kuwa mwanahabari huyo yumo kujaribu kupiga sim ya mwanamuziki huyo ili kuhojiana na yeye kuhusiana na hali ya jana nakuwa anaimani muda huyu pombe zitakuwa zimemtoka.
Swali kuu ambalo mwanahabari huyu anajiuliza je,hawa ndo viyo vya jamii ambao wanao paswa kuigwaaaaaa?




TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi