Mwili wa Daktari mwingereza Abbas Khan
aliyefariki dunia akiwa gerezani nchini Syria, umekabidhiwa kwa familia
yake na maafisa wa Uingereza nchini Lebanon jana Jumamosi huku familia
ikidai kuwa serikali ya Syria imehusika na kifo chake.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human
Rights Watch pia limeweka shinikizo kwa mamlaka nchini Syria,
likiishutumu serikali kwa kusababisha maafa kutokana na mashambulizi ya
anga kwenye mji wa Aleppo.
Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) na Shirika la Msalaba
Mwekundu la nchini Lebanon wamesindikiza mabaki ya mwili wa Khan kutoka
Syria hadi Lebanon kwa msafara wa magari matatu.
Katika juhudi za kidiplomasia , mjumbe wa amani Lakhdar Brahimi amefanya mazungumzo na waziri wa mambo ya kigeni wa Iran, baada ya wasuluhishi kushindwa kukubaliana kuhusu umuhimu wa Tehran kwenye mkutano wa amani.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!