Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KATI YA WAGOMBEA WA KITI CHA URAIS NCHINI MADAGASCAR KILA MMOJA ADAI MSHINDI KWENYE UCHAGUZI WA DURU YA PILI

KATI YA WAGOMBEA WA KITI CHA URAIS NCHINI MADAGASCAR KILA MMOJA ADAI MSHINDI KWENYE UCHAGUZI WA DURU YA PILI

Written By Unknown on Monday, 23 December 2013 | Monday, December 23, 2013

Matokeo ya awali ya duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Madagascar yanampa ushindi mgombea wa utawala uliopo nchini humo, Hery Rajaonarimampianina. Mgombea huyo amejigamba kuwa anaimani kuwa ataibu mshindi katika uchaguzi huo ambao matokeo ya awali yanampa ushindi.
Kulingana na matokeo ya muda ya duru ya pili ya uchaguzi ulioffanyika siku ya Ijumaa Desemba 20 iliopita, takriban asilimia 15 ya kur ambazo tayari zemehesabiwa, mgombea Rajaonarimampianina anaongoza kwa asilimia 53.6 ya kura hizo.
Mgombea huyo ameilalamika kuwepo na udanganyifu katika uchaguzi huo, kwani amesema angelipata kura zaidi ya hizo, huku msemaji wake, Rinah Rakotomanga, akibaini kwamba Rajaonarimampianina ameshinda kwa asilimia kati ya 60 na 65 ya kura.
Mpinzani wake Robinson Jean Louis, anaye ungwa mkono na rais wa zamani wa taifa hilo Marc Ravalomanana, amesema kuwa uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa kura, na kudaikuwa ameibuka mshindi, baada ya timu yake kuhesabu asilimia 80 ya kura alizoshinda nchini kote.
Robinson Jean Louis alifahamisha juzi Jumamosi kwamba alipata asilimia 56 ya kura.
Robinson Jean Louis, aliomba siku ya ijumaa, kusitisha kutangaza matokeo ya uchaguzi ya duru ya pili, akibaini kwamba ni mbinu za kutaka kumuibia ushindi wake.

Kauli hiyo imetupiliwa mbali na mpinzani wake Hery Rajaonarimampianina ambaye amesema kwamba anao ushahidi wa kutosha unaoonyesha jinsi alivyoibiwa kura.
Waangalizi wa kimataifa wamesema wameridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika. Mpaka sasa waangalizi wa kimataifa wakiwemo wale wa Umoja wa Ulaya hawajathibitisha uwepo wa wizi wa kura au la.
Mkuu wa ujumbe waangalizi wa Umoja wa Ulaya, Maria Muniz de Urquiza, amesema uchaguzi huo umekua huru , wa kweli na wa wazi.
Mchakato bado unaendelea, shughuli ya kuhesabu kura inaendelea huku mshindi wa uchaguzi huo akitarajiwa kutangazwa mwanzoni mwa mwezi januari mwakani.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi