Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » KUNDI LA KUTETEA HAKI ZA BINADAM NCHINI ANGOLA LA LAANI SHOW YA MARIA CAREY ALIYO IFANYA NCHINI HUMO,LIKIDAI ALILIPWA PESA ZA KIFISADI

KUNDI LA KUTETEA HAKI ZA BINADAM NCHINI ANGOLA LA LAANI SHOW YA MARIA CAREY ALIYO IFANYA NCHINI HUMO,LIKIDAI ALILIPWA PESA ZA KIFISADI

Written By Unknown on Sunday, 22 December 2013 | Sunday, December 22, 2013

Hivi karibuni Mariah Carey alizikonga nyoyo za mashabiki huko Angola kwa show ya maana iliyomuingizia kiasi cha dola za Marekani Milioni 1, sawa na bilioni 1 na milioni 600 za Burundi.
Kundi la kutetea haki za binadamu ‘Human Right Foundation’ limemkosoa vikali mwimbaji huyo kwa madai kuwa alikubali kulipwa fedha na binti wa rais wa Angola Jose Eduardo dos Santos, rais ambaye anatuhumiwa na baadhi ya makundi ya kutetea haki za binadamu kuwa fisadi.
Mariah Carey alipiga show ya masaa mawili nchini Angola iliyoandaliwa na Red Cross ya nchini humo, na kampuni ya simu ya Unitel ambayo inamilikiwa na binti wa rais Dos Santos aitwae Isabel.


Pia Isabel ndiye rais wa Red Cross nchini Angola.
Rais wa Human Right Foundation aitwae Thor Halvorssen ameandika tamko linalomkosoa Mariah Carey, “Mariah Carey haonekani kutosheka na pesa za dictator, imeripotiwa amelipwa dola milioni 1 kipindi hiki. Miaka mitano tu iliyopita aliperform kwenye familia ya dictator wa Libya Muammar Gaddafi.”
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi