Mapigano kwa sasa yanashuhudiwa katika miji ya Bor, katika Jimbo la Jonglei na Torit katika jimbo la Eastern Equatoria.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa unakadiria kati ya watu 400 na 500 wamepoteza maisha tangu jaribio hilo la kuipundua serikali ambalo rais Kiir anamtuhumu aliyekuwa Makamu wake Riek Machar kupanga jaribio hilo tuhma ambazo Machar amekanusha.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amesema njia pekee ya kutatua mgogoro huu ni mazungumzo.
Ban amewataka wahusika katika mzozo huu kuketi pamoja ili kuepuka hatari ya kuenea kwa mapigano hayo katika nchi za jirani.
Wito wa Ban unakuja huku rais Salva Kiir akisema kuwa yuko tayari kuzungumza na Riak Machar ambaye hajulikani aliko.
Hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa mjini Juba na viunga vyake huku wageni wakitafuta hifadhi katika ofisi za Umoja wa Mataifa.
Migawanyiko imeanza kushudiwa katika chama tawala, jeshini, na kumekueko na hofu ya kutanda kwa uhasama wa kikabila katika nchi hio ambayo bado ni changa.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!