MENEJA wa klabu ya Paris
 Saint-Germain, Laurent Blanc ameonya kikosi chake kuwa kinatakiwa kuwa 
makini wanapokuwa mwa adui baada ya kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 
na Lille. Blanc pia amedai kuwa wahezaji wake hawapaswi kumtegemea moja 
kwa moja mshambuliaji nyota wa klabu hiyo Zlatan 
Ibrahimovic. Ibrahimovic alifunga bao la kuongoza kwa timu yake dakika 
ya 27 lakini Lille walikuja juu na kurudisha bao hilo kupitia kwa Rio 
Mavuba kabla ya Salomon Kalou hajaongeza lingine huku PSG wakisawazisha 
kupitia bao la kujifunga la Marko Basa na kupelekea timu hizo kugawana 
alama moja kila mmoja. Mara baada ya mchezo huo Blanc alikitaka kikosi 
chake kutowategemea sana Ibrahimovic na Edinson Cavani ambaye alikosa 
mchezo huo kwasababu binafsi. Blanc amesema pamoja na kufurahishwa na 
kiwango bora walichokionyesha lakini matokeo hayakumridhisha kwasababu 
kuna nafasi nyingi walizokosa ambazo kama wangezitumia vyema wangeweza 
kuibuka na ushindi katika mchezo huo. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa 
wachezaji wote wanatakiwa kuwa makini pindi wafikapo langoni mwa adui na
 sio kuwategemea moja kwa moja Ibrahimovic na Cavani.
Home »
michezo ulaya
 » LAURENT BLANC ATOWA USHAURI KWA WACHEZAJI WAKE KUWA WASIMTEGEMEI SANA IBRAHIMOVIC
LAURENT BLANC ATOWA USHAURI KWA WACHEZAJI WAKE KUWA WASIMTEGEMEI SANA IBRAHIMOVIC
Written By Unknown on Monday, 23 December 2013 | Monday, December 23, 2013
Labels:
michezo ulaya



0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!