Mgombea wa Uchaguzi wa rais nchini Madagascar Jean Louis Robinson anataka zoezi la kuhesabu na kujumuisha kura kusitishwa.
Robinson anasema haamini kuwa zoezi hilo linakwenda vizuzri kwa kile anachosema kuna wizi mkubwa wa kura unaoendelea.
Hata hivyo, tume ya Uchaguzi inasema inafanya kila kilicho
ndani ya uwezo wake kutoa matokeo sahihi na yeyote asiyeridhika aende
Mahakamani.
Beatrice Atallah rais wa tume ya Uchaguzi nchini Madagascar, Jean Louis Robinson, ana haki ya kufika mahakamani.
“Nimemuomba binti yake aniwasilishie nyaraka za matokeo, kwa sababu kila mgombea ana nyaraka hizo, ili tuweze kulinganishaa kabla ya kufikisha malalamiko yake mahakamani, na anatakiwa afanye hivo ndani ya siku kumi baada ya uchaguzi”, amesma Atallah.
Kinyan'ganyiro kikali ni kati ya Jean Louis Robinson na Hery Rajaonari mampianina anayeonekana kuwa katika nafasi nzuri ya kushinda.
Jumuiya ya Kimataifa na Umoja wa Afrika uliwataka marais wazamani wa nchi hio kutogombea kwenye kiti cha urais kutokana na tofauti zao.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!