MJANE wa marehemu Sheikh Aboud Rogo Alhamisi aliambia mahakama ya Mombasa kwamba haoni sababu za jopo kuundwa kuchunguza mauaji hayo.
Bi Haniya Said Sagar alimweleza hakimu mkuu wa Mombasa, Bw Stephen Riechi kwamba anaonelea heri ni aachwe aendelee kuwalea watoto wake, badala ya kuitwa mahakamani kutoa ushahidi katika jopo la uchunguzi wa mauaji ya mumewe.
“Uchunguzi huu hauna maana yoyote maana hautaweza kumfufua marehemu mume wangu na badala yake ni kufungua kovu la kidonda. Sitaki kuitwa tena kutoa ushahidi,” Bi Haniya akaeleza mahakama.
Bw Alexander Muteti, mwendesha mashtaka mkuu kutoka afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma alieleza mahakama kwamba mashahidi 29 wanatazamiwa kutoa ushahidi, akiongezea kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka iwapo kutakuwa na watu wenye ushahidi dhidi mauaji ya kinyama ya Sheikh Rogo.
Mahakama itaendelea kukusanya ushahidi mnamo Februari 20, 2014
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!