Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » MWANAMUZIKI MKONGWE KUTOKA CONGO DRC BW TABULEY AAGA DUNIA

MWANAMUZIKI MKONGWE KUTOKA CONGO DRC BW TABULEY AAGA DUNIA

Written By Unknown on Monday, 2 December 2013 | Monday, December 02, 2013

Tabu Ley Rochereau, mwanamuziki maarufu na mwanzilishi wa mtindo wa rumba wa soukous akijulikana kama"Mfalme wa Rumba la Congo" ambaye alikuwa mmoja wa wanamuziki waliopendwa barani Afrika, amefariki Jumamosi katika hospitali moja mjini Brussels, Ubelgiji.
Mwanamuziki huyo akiitwa Pascal-Emmanuel Sinamoyi Tabu alizaliwa wakati wa utawala wa Wabelgiji nchini Congo mwaka 1937 au 1940, kutegemea na vyanzo vya habari, alikuwa akiumwa tangu mwaka 2008 akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi. Kiongozi wa bendi ya Orchestre Afrisa International alikuwa ni kiongozi mbunifu ambaye uimbaji wake uliunganisha sauti za muziki wa Kiafrika, Cuba,na mirindimo ya Caribbean, na aliimba bila kuchoka na kubandikwa jina la "Sauti ya Mwangaza."
Muziki wa Tabu Ley unapatikana katika mamia ya santuri za LP. Miongoni mwa santuri hizo ni ile ya Ley, Ley, Seigneur Ley Rochereau. Pia kwa weledi mkubwa kazi zake zimekusanywa katika CD.
Mwanamuziki Tabu Ley ambaye alikuja kushirikiana kimuziki na hata kimapenzi na mwanamuziki wa kike kutoka huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Mbilia Bel, alitikisa anga ya muziki wa rumba duniani, na hususan eneo la Afrika Mashariki na Kati.
Kwa mfano mwaka 1987 alifanya ziara nchini Tanzania, wakiwa na Mbilia Bel na kutembelea mikoa kadha, ikiwa ni kusherehekea miaka kumi ya kuzaliwa kwa chama tawala cha CCM, nchini Tanzania.
Miongoni mwa vibao vilivyompa umaarufu mkubwa Tabu Ley ni Muzina, Maze, C'est comme ca la vie, selikutu, Ibeba, Nadina na nyingine nyingi.
Wapenzi wa muziki wa rumba, watamkosa Tabu Ley, lakini wataendelea kuburudika na nyimbo zake ambazo alizitunga katika uhai wake, akiwa mwanamuziki.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi