MENEJA wa klabu ya
Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amekiri kuwa kikosi chake kinahitaji
mapumziko ya majira ya baridi baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1
kutoka Hertha Barlin jana. Dortmund wamekuwa wakisumbuliwa na majeruhi
katika mzunguko wa kwanza wa ligi msimu huu ambapo sasa wako nyuma ya
vinara wa Bundesliga Bayerm Munich kwa alama 12. Kipigo hicho cha jana
walichopata nyumbani kinakuwa cha tatu mfululizo na Klopp sasa
anajipanga kurejesha makali ya timu yake ambayo yamepotea kutokana na
majeruhi ya wachezaji yaliyomwandama. Klopp amekiri kuwa wanahitaji
mapumziko ili kujipanga na kuangalia mapungufu yao ili waweze kurejea
katika kiwango chao.
Home »
michezo ulaya
» NAONA KIKOSI CHANGU KIMEANZA KUCHOKA SASA TUNAHITAJI MAPUMZIKO YAKUTOSHA:JURGEN
NAONA KIKOSI CHANGU KIMEANZA KUCHOKA SASA TUNAHITAJI MAPUMZIKO YAKUTOSHA:JURGEN
Written By Unknown on Sunday, 22 December 2013 | Sunday, December 22, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!