Rais wa Marekani Barack Obama jana
Jumamosi amevionya vikosi vya waasi nchini Sudan Kusini dhidi ya
mapinduzi ya kijeshi baada ya wanajeshi wanne wa Marekani kujeruhiwa
katika shambulizi dhidi ya ndege yao wakati wakijielekeza mjini Bor kwa
shughuli za uokozi.
Taarifa ya ikulu ya Marekani imeeleza kuwa juhudi zozote za kunyakua
madaraka kwa nguvu za kijeshi zitasababisha kukoma kwa msaada wa muda
mrefu kutoka Marekani jumuiya ya kimataifa.Rais Obama amesisitiza kuwa viongozi wa Sudani Kusini wanalo jukumu la kusaidia juhudi za Marekani kuwaokoa wamarekani na raia huko Juba na Bor mji ambao unashikiliwa na waasi.
Onyo la rais Obama linakuja baada ya ndege tatu za Marekani kushambuliwa kwa risasi wakati zikielekea huko Bor kusaidia juhudi za kuwaondoa wa Marekani nchini Sudani Kusini kufuatia kuchacha kwa mapigano baina ya serikali na waasi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!