STRAIKA hatari wa Manchester City, Sergio Aguero ameipa pigo klabu yake baada ya kuripotiwa kwamba atakuwa nje ya uwanja kwa takribani mwezi mmoja.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Manuel Pellegrini alibainisha kwamba straika wake hataonekana uwanjani kwa muda huo baada ya kuumia katika mechi ya Ligi Kuu ya England ya ushindi wa mabao 6-3 dhidi ya Arsenal Jumamosi iliyopita.
Staa huyo wa Argentina ndiye kinara wa mabao wa Manchester City baada ya kufunga mabao 19 msimu huu, mabao 13 akiyafunga kwenye Ligi Kuu England.
Pellegrini alithibitisha kwamba atamkosa Aguero kwa mwezi mzima wakati alipozungumza na waandishi wa habari jana Jumatatu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!