Rubani wa ndege ya shirika la Ethiopia Airlines iliyotua kwa dharura kwenye uwanja wa ndege wa Arusha, alitua kwenye uwanja huo baada ya kudhania ni ule wa Kilimanjaro International Airport (KIA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini Tanzania, (TCAA) imesema.
Badala yake rubani huyo alitua kwenye uwanja wa ndege wa Arusha wenye njia ya kutua iliyo na urefu wa meta 1,640 ambayo ni fupi mno kwa ndege hiyo aina ya Boeing 767-300ER kutua. Ndege hiyo inahitaji walau njia ya kutua yenye urefu wa meta 1,798.
Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Fadhil Manongi, alisema kwenye maelezo yake kuwa pamoja na kwamba kulikuwa na ndege mbovu kwenye njia ya kutua ndege ya KIA, uwanja huo una njia yenye urefu wa meta 3,600 na kusema kuwa bado kulikuwa na meta 3,200 zilizotosha kwa ndege No. ET-815 kutua.
Amesema tayari wataalam wapo uwanjani hapo kufanya uchunguzi.
Meneja wa Uwanja wa Ndenge wa Arusha, Ester Dede alisema baada ya abiria wote 213 waliokuwa katika ndege hiyo kusaidiwa na kuendelea na safari zao, uchunguzi umeanza kubaini chanzo cha tukio hilo.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!