Staa huyo wa Uskochi aliyeanza kuugua Novemba 2011, juzi Jumapili alirejea uwanjani wakati alipocheza dakika 20 za mwisho kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambapo Manchester United iliinyuka Aston Villa mabao 3-0.
“Nimerudi uwanjani kutoka kwenye vikwazo vingi vya kiafya na nashukuru Mungu kwa hilo. Kutoka sasa ni mbele kwa mbele. Siku zote niliamini nitarejea uwanjani, nilijiandaa hivyo. Watu niliokuwa nao walikuwa wakinishauri tofauti, lakini nilikuwa na mipango yangu.
“Tangu nilipokuwa mtoto, nilihitaji kucheza soka. Nimekuwa na bahati sana kwa kucheza Manchester United na hivyo nisingeweza kukata tamaa kirahisi. Nimepambana sana, umri wangu ni miaka 29 tu hivyo naamini bado nina muda wa kutosha.”
Fletcher hakuwa amecheza mechi yoyote ya kikosi cha kwanza cha Manchester United tangu baada ya ushindi wa mabao 4-3 dhidi ya Newcastle United Desemba mwaka jana.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!