Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SERIKALI YA SUDAN KUSINI IMESEMA INAAMINI KUWA KUNA MIJI KADHAA IPO MIKONONI MWA WAASI WA RIEK MASHAR

SERIKALI YA SUDAN KUSINI IMESEMA INAAMINI KUWA KUNA MIJI KADHAA IPO MIKONONI MWA WAASI WA RIEK MASHAR

Written By Unknown on Monday, 23 December 2013 | Monday, December 23, 2013


Serikali ya Juba imesema waasi wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa majimbo ya Joglei na Unity huku maelfu ya watu wakikimbilia katika Mako Makuu ya Umoja wa Mataifa kupata hifadhi. Wakati hayo yanajiri, Rais wa Marekani Barrack Obama amesema kuwa hatua zaidi zitachukuliwa nchini Sudan Kusini iwapo makabiliano zaidi yataendelea kushuhudiwa nchini humo baada ya ndege yake ya kijeshi kuvamiwa mwishoni mwa juma lililopita.

Kauli ya rais Obama inakuja kipindi hiki Jumuiya ya Kimataifa ikiendelea na juhudi za Kidiplomasia kujaribu kuleta utulivu nchini humo na Umoja wa Mataifa unaahidi kutuma wanajeshi zaidi wa kulinda amani. Mataifa ya Uingereza, Marekani, Kenya, Lebanon na Uganda yamekuwa yakiwaondoa raia wake waliopata hifadhi katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa kutokana na makabiliano hayo ya kijeshi.
Mwishoni mwa juma lililopita jeshi la Kenya limefanikiwa kuwarudisha nyumbani wakenya zaidi ya themanini pamoja na kupeleka msaada wa vyakula na dawa kwa watu waliokimbilia katika kambi ya Umoja wa Mataifa.
Zaidi ya watu mia tano wameuawa nchini Sudan Kusini tangu yatokeye makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali na wale wanaomuunga mkono aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar ambaye anasema anataka kuwa rais wa nchi hiyo.
Juma lililopita baadhi ya mawaziri wa Mambo ya nje kutoka nchi za kiafrika walikuwa jijini Juba kushauriana na rais Salva Kiir kujaribu kupata suluhu la kisiasa kati yake na Riek Machar bila mafanikio.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi