MSHAMBULIAJI wa
kimataifa wa Argentina amedai kuwa hana matumaini ya kuitwa katika
kikosi cha nchi hiyo kitakachoshiriki michuano ya Kombe la Dunia
mwakani. Tevez mwenye umri wa miaka 29 ambae amekuwa katika kiwango
kizuri msimu huu ambapo ameifungiwa timu yake ya Juventus mabao 10,
amekuwa akiachwa katika kikosi cha nchi yake toka Alejandro Sabella
alipotwaa mikoba ya kuinoa Argentina Agosti mwaka 2011. Akihojiwa Tevez
amesema kama Sabella hatamwita katika kikosi chake, hana mpango wa
kumpigia simu na kumhoji kwanini hajamwita kwasababu anataka aifanye
kazi yake kwa weledi. Nyota huyo wa zamani wa vilabu vya Manchester
City, Manchester United na West Ham United amesema ana mahusiano mazuri
na wachezaji wote wa Argentina pamoja na nahodha wao Lionel Messi, hivyo
suala la yeye kuitwa au kutokuitwa ni juu ya kocha mwenyewe. Argentina
ambao ni mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka 1978 na 1986 wamepangwa kundi F
sambamba na timu za Bosnia, Iran na Nigeria.
Home »
michezo ulaya
» SINA MATUMAINI KAMA NTAITWA KWENYE KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA:TEVEZ
SINA MATUMAINI KAMA NTAITWA KWENYE KIKOSI CHA TIMU YA TAIFA YA ARGENTINA:TEVEZ
Written By Unknown on Sunday, 22 December 2013 | Sunday, December 22, 2013
Labels:
michezo ulaya
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!