Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » TIMU YA TAIFA YA UINGEREZA HAITACHEZA ULE MCHEZO KAMA WA ARSENAL WA "TIK TAK"

TIMU YA TAIFA YA UINGEREZA HAITACHEZA ULE MCHEZO KAMA WA ARSENAL WA "TIK TAK"

Written By Unknown on Tuesday, 10 December 2013 | Tuesday, December 10, 2013

 
KILA ligi barani Ulaya inatambuliwa kwa jinsi timu katika ligi hizo zinavyocheza mpira. Kwa mfano, timu za Ujerumani zinacheza mpira tofauti na timu za Hispania.
Timu za taifa huwa zinacheza mpira unaofanana na ule ambao timu nyingi zinacheza katika ligi kuu ya nchi hiyo.
Kwa mfano, timu ya taifa ya Italia huwa wanacheza fomesheni ya 3-5-2.
Ni kwa kuwa Juventus ambao ni mabingwa wa Italia wanacheza na fomesheni hii. Na Juventus wana wachezaji wengi wanaocheza katika timu ya taifa ya Italia.
Kama Italia hawachezi fomesheni ya 3-5-2, basi watacheza fomesheni ya 4-3-3. Ni kwa kuwa timu nyingi katika ligi ya Italia zinacheza kwa kutumia fomesheni hii.
 
Vile vile, timu ya taifa ya Hispania inacheza mpira wa staili ya “tiki taka” Staili hii ina maana timu inacheza mpira wa kushambulia kwa kuumiliki mpira kwa muda mrefu na wakati huo huo kupiga pasi nyingi.
Hispania wanacheza mpira huu kwa kuwa katika Ligi Kuu Hispania au La Liga, timu nyingi zinacheza mpira wa staili ya “tiki taka” au aina ya mpira inayofanana na “tiki taka”.
Kwa hiyo, inakuwa rahisi kwa wachezaji wanaocheza katika Ligi Kuu Hispania kucheza katika timu ya taifa ya Hispania. Ni kwa kuwa jinsi ya kucheza staili hiyo inafanana.
Klabu nyingi za Ujerumani zinacheza mpira wa kushambuliana, vile vile, timu ya taifa ya Ujerumani inacheza mpira unaofanana na ule ambao Bayern Munich, Borrusia Dortmund na Schalke 04 inacheza.
Mabingwa wa England, Manchester United wana wachezaji saba wanaocheza timu ya taifa ya England, lakini wengi wao hawapo katika kikosi cha kwanza cha timu ya taifa ya England. Wachezaji kama Ashley Young na Chris Smalling.
Timu ya taifa ya England inacheza mpira unaofanana na ule ambao Manchester United inaucheza, lakini katika miaka ya karibuni, timu nyingi za Uingereza zimeanza kujaribu kucheza mpira unaofanana na ule ambao timu za Hispania na timu ya taifa ya Hispania inaucheza.
Kwa kutumia staili hii, timu ya taifa ya Hispania na timu za Hispania zimepata mafanikio makubwa. Kwa hiyo, timu nyingi za Uingereza zinanunua wachezaji wanaocheza katika ligi kuu ya Hispania.

Na ndio maana katika misimu ya karibuni, wachezaji wengi kutoka Ligi Kuu Hispania wamesajiliwa na katika timu za Ligi Kuu England.
Wachezaji kama Santi Cazorla, Juan Mata, David Silva, Michu, Negredo, Soldado, Agüero na Jesus Navas.
Timu nyingi za England zimeanza kucheza mpira unaofanana na ule wa Hispania. Lakini, sidhani kwamba timu ya taifa ya England itacheza mpira wa staili ya ‘tiki taka’.
Ni kwa kuwa katika timu ambazo zinacheza mpira unaofanana na “tiki-taka” kama Manchester City, Waingereza wapo wachache na hawamo katika kikosi cha kwanza cha timu husika.
Kwa maana nyingine kuutumia mfumo huu ni sawa na kuivuruga timu ambayo wachezaji wake wanajikuta katika wakati mgumu.
Hususan katika kipindi hiki ambacho timu zinajinoa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil ni muhimu kwa timu kujipanga na kutumia mfumo ambao utakuwa na maana kwa timu nzima kwa maana ya kwamba wachezaji wote watafiti katika mfumo huo na hivyo kuwa na msaada kwa timu yao.
Itakuwa kosa kubwa kutumia mfumo ambao unatumiwa na klabu fulani wakati sehemu kubwa ya wachezaji hawatokei katika klabu hiyo au ni wachache wanaomudu mfumo wa aina hiyo.
Na kwa kuwa timu ya taifa inaandaliwa kwa muda mfupi suala la mfumo gani unafaa lina umuhimu wa kipekee kwa makocha wa timu husika.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi