Hali ya
wasiwasi imeendelea kushuhudiwa katika Jimbo lenya utajiri wa mafuta la
Unity ambalo kwa sasa lipo chini ya wanajeshi wanaomuunga mkono
aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar. Serikali ya Juba inasema jeshi la
serikali kwa sasa linajiandaa kuwashambulia waasi hao ili kuchukua tena
udhibiti wa mji huo muhimu kutokana na utajiri wake wa mafuta. Wakati
huo huo Kamanda wa Jeshi la serikali katika Jimbo hilo amejitangaza kuwa
Gavana wa jimbo hilo.
Kwa sasa hali ni ya wasiwasi katika majimbo hayo huku wageni wakiendelea kurudi makwao kwa hofu ya kushambuliwa.
Rais Salva Kiir ameliambia bunge la nchi hiyo kwamba majeshi yapo tayari na kuongeza kuwa mashambulizi yalicheleweshwa ili kuruhusu raia kuondolewa katika majimbo hayo
Bor, ni eneo lililokuwa na mgogoro ambalo lipo ndani ya jimbo la Jonglei lililoangukia mikononi mwa waasi siku ya jumatano.
Takribani wiki imepita tangu mapigano ya kikabila yaanze na kusababisha hofu kwa raia. Maafisa wa shirika la misaada wamelielezea eneo hilo kuwa na matukio ya umwakigaji damu pamoja na mauaji.
Nalo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linataka kufanyika mazungumzo ya haraka ili kumaliza mapigano yanayoendelea.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataufa Ban Ki Moon amesema kuwa atawasilisha ombi kwa Baraza la Usalama kuomba wanajeshi zaidi wa kulinda amani kutumwa nchini Sudan Kusini.
Aidha, Moon ameonya kuwa yeyote atakayepatikana kuchochea mapigano hayo atafunguliwa mashataka ya ukiukwaji wa Haki za Bianadamu.
Kwa wiki ya pili leo, majeshi yanayomuunga mkono rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wa rais Riek Machar yameendelea kupambana na kusabibisha mamia ya watu kuuawa na maelfu kukimblia katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa wanakopata hifadhi.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!