Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » USALAMA WA ISRAEL NI WAMUHIMU KWANZA KWENYE MAZUNGUMZO NA IRAN

USALAMA WA ISRAEL NI WAMUHIMU KWANZA KWENYE MAZUNGUMZO NA IRAN

Written By Unknown on Thursday, 5 December 2013 | Thursday, December 05, 2013

Waziri wa mammbo ya kigeni wa Marekani John Kerry amesisitiza kuwa usalama wa Israel ni kipaumbele cha kwanza kwenye mazungumzo na Iran kuhusu mpango wake tata wa Nyuklia baada ya makubaliano ya awali kutiwa saini.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu leo Alhamisi mjini Yerusalem, Kerry amesema kuwa anaendelea kusisitiza kuwa usalama wa Israel ni muhimu na Marekani itafanya lolote ndani ya uwezo wake kuhakikisha kwamba mpango Nyuklia wa Iran na silaha za maangamizi lazima ukomeshwe.
Kauli ya Kerry inalenga kutuliza mvutano na Israel kuhusu mpango wa mpito uliofikiwa mjini Geneva Uswisi mnamo Novemba 24 , mpango ambao ulishuhudia Iran ikikubali kusitisha baadhi ya sehemu za mipango yake ya Nyuklia kwa lengo la kurahisishiwa vikwazo vya mataifa ya Magharibi.
Makubaliano hayo yalilaaniwa vikali na Waziri mkuuwa Israel Benjamin Netanyahu, ambaye aliyaita kosa la kihistoria.
Kerry amewasili Israel jana usiku kwa ziara inayolenga kuyapa nguvu mazungumzo ya amani kuhusu Israel na Palestina, mazungumzo ambayo yamepata mafanikio haba tangu kuanza kwake mwezi Julai chini ya usimamizi wake .
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi