Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » , » SOMA ALIVYO JIBU MWANAMUZIKI DAVIDO,BAADA YAKUULIZWA SWALI KUHUSU NINI ATAFANYA MWAKA HUU WA 2014

SOMA ALIVYO JIBU MWANAMUZIKI DAVIDO,BAADA YAKUULIZWA SWALI KUHUSU NINI ATAFANYA MWAKA HUU WA 2014

Written By Unknown on Wednesday, 22 January 2014 | Wednesday, January 22, 2014

Mwimbaji aliyeandika historia nzuri katika muziki wake mwaka jana kwa mafanikio makubwa aliyoyapata kutokana na hit yake ya ‘Skelewu’, Davido, mwaka huu soko la mauzo ya album halitaupata mzigo mpya toka kwake.
Mkali huyo toka Naija amefunguka kupitia twitter alipokuwa akijibu maswali ya mashabiki wake waliotaka kujua mwaka huu amejipanga vipi na kama kweli ataachia album mpya au la!
Amesema kwamba atajikita zaidi katika kuhakikisha mafanikio ya wasanii wa label yake ya HKN Music,  ili wote wachomoke na sio kuona yeye peke yake akichomoka.
“This year I’m focused on the success of my Artists and Label!! No only me go blow! We all must chop!!! Hkn Gang!” Alitweet Davido.
Aliweka wazi katika tweet nyingine kuwa hatatoa album mpya mwaka huu.
Hata hivyo, mkali huyo ameretweet ujumbe ulioandikwa na fan wake kukanusha habari kuwa watu wasitegemee mengi toka kwake, bali wataendelea kusikia nyimbo na kuona videos toka kwake. Kinachokosekana ni album tu. Je, mwaka huu tutapata ngoma kali kama Skelewu toka kwa Davido? Tuendelee kusubiri, bado mapema.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi