JOTO kali lililopo
katika jiji la Melbourne limesababisha kusimamishwa kwa michuano ya
tenisi ya wazi ya Australia kwa masaa manne. Baadhi ya michezo ambayo
ilikuwa ichezwe katika viwanja vya wazi ilishindikana kutokana na joto
kuzidi na kufikia nyuzi joto 43 hatua ilipelekea waandaaji kusogeza
mbele mpaka muda wa jioni ambao joto huwa linapoa kidogo.
Pamoja na baadhi ya
viwanja kusimama lakini viwanja vingine katika michuano hiyo kama Rod
Laver Arena na Hisense mechi zake ziliendelea kama kawaida baada ya
kufunikwa juu ya paa na kuwashwa vipoza hewa. Jumanne waandaji wa
michuano hiyo walishambuliwa kwa kuruhusu wachezaji kucheza katika joto
kali hatua iliyopelekea wengine kuzidiwa na kuanguka.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!