Borussia Dortmund CEO
Hans-Joachim Watzke ametoa tuhuma kwamba mahasimu wao Bayern Munich
wana lengo la kuidhoofisha timu yake kwa kuwasajili wachezaji wao
muhimu.
Bayern tayari imeshamsajili Mario Gotze kutoka BVB na hivi karibuni wametangaza kwamba Robert Lewandowski atajiunga na timu yao akitokea Dortmund mwezi June mwaka huu.
Watzke anaamini kwamba utawala wa Bayern umeifanya Bundesliga kuwa michuano ya timu moja na kusisitiza kwamba kikosi cha Pep Guardiola kina nia ya kuzuia timu kama Dortmund kukua na kuwa tishio kwao baadae.
"Hakuna ligi yoyote sasa hivi inayotawaliwa na klabu moja kama ilivyo hapa kwa Bayern ndani ya Bundesliga. Hali ya hapa sio kama ya ligi ya Hispania, au Uskochi," Watzke aliwaambia wandishi wa habari.
"Bayern sasa wanafanya kisasi baada ya Dortmund kutwaa ubingwa mara mbili mfululizo. Wantaka kutuharibia timu ili kuhakikisha hatuji kuwa tishio tena.
"Na wanafanya hivyo kwa kuwasajili wachezaji wetu.
"Hatuwezi kufanya lolote kuwazuia wachezaji wetu kwenda mahala ambapo wanaahaidiwa mishahara mara mbili tunayowalipa. Pamoja na yote haya, hatutobadili mbinu zetu."
Watzke aliendelea na kusema kwamba Dortmund haitosita kusajili vizuri mwishoni mwa msimu ili kuwa tayari kushindania ubingwa wa Bundesliga msimu ujao.
"Tutawekeza kwa kiasi kikubwa wakati wa kiangazi na hatuzungumzii fedha kidogo, tutasajili kwa fedha nyingi tu wakati wa kiangazi. Tutafanya hivyo kwa kuzingatia bajeti yetu."
Bayern mpaka sasa wanaongoza kwa pengo la pointi 13 mbele ya Bayer Leverkusen katika Bundesliga, huku Dortmund wakiwa nyuma kwa pointi 17 katika nafasi ya 3.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!