MSHAMBULIAJI mkorofi wa AC Milan, Super Mario Balotelli amesema
bao la ushindi alilofunga katika pambano dhidi ya Verona juzi Jumapili
ni zawadi kwa kocha wake mpya, Clarence Seedorf.
Milan walilazimika kusubiri mpaka dakika za
majeruhi kufunga bao la penalti kupitia kwa staa huyo wa zamani wa
Manchester City, wakati huu hali yao ikiwa mbaya kwao katika msimamo wa
ligi.
“Nampongeza kocha? Ndiyo, ushindi huu ni kwa ajili
yake. Ilikuwa ni mechi yake ya kwanza na ni wazi kwamba hali ilikuwa
ngumu. Tulijipanga vizuri na tulicheza vyema,” alisema Balotelli. Mechi
ya pili ya Seedorf kwa Milan itakuwa dhidi ya Udinese kesho Jumatano
katika pambano linalotarajiwa kuwa kali na la kusisimua ambalo litakuwa
kipimo kwa kocha huyo Mdachi.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!