Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » KAMA ULIKUWA HAUFAHAMU BASI HIZI NDIZO HISTORIA ZA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHAA ILIOPITA

KAMA ULIKUWA HAUFAHAMU BASI HIZI NDIZO HISTORIA ZA SIKU KAMA YA LEO MYAKA KADHAA ILIOPITA

Written By Unknown on Thursday, 23 January 2014 | Thursday, January 23, 2014

Siku kama ya leo miaka 35 iliyopita kutokana na kukaribia ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran, kamati ya uratibu iliundwa nchini humo lengo likiwa ni kuzuia hali ya hofu na vitisho. Kamati hiyo iliwatolea mwito wafanyakazi na wananchi wote kuendelea na migomo na maandamano yao hadi kufikia ushindi kamili wa Mapinduzi ya Kiislamu. Katika siku hiyo pia vikosi vya usalama viliondolewa katika mji wa kidini wa Qum nchini humo na badala yake mji huo ukawa chini ya udhibiti wa wananchi.
Miaka 64 iliyopita mwafaka na tarehe 23 Januari 1950 Bunge la utawala wa Kizayuni wa Israel kwa jina la Knesset liliitangaza Baitul Muqaddas ambayo ni kibla cha kwanza cha Waislamu kuwa mji mkuu wa utawala huo. Uamuzi huo wa Bunge la utawala ghasibu unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu ambao ulichukuliwa miaka miwili baada ya kuasisiwa utawala huo bandia katika ardhi za Palestina, ulizusha hasira na upinzani mkubwa wa Waislamu. Hata hivyo jitihada za utawala haramu wa Israel kwa lengo la kuzishawishi nchi nyingine ziunge mkono suala la kutambuliwa rasmi Baitul Muqaddas kuwa mji mkuu wa utawala huo na pia kuhamishia balozi zao katika mji huo, hazijazaa matunda na hadi sasa Tel Aviv inaendelea kutambuliwa kama mji mkuu wa utawala ghasibu wa Israel.
Siku kama hii ya leo miaka 95 iliyopita chama cha Kifashisti cha Taifa cha Italia kiliundwa na Benito Mussolini. Wanachama wa chama hicho walikuwa wakitaka kufanyiwa marekebisho mfumo wa utawala wa kifalme wa Roma na walifahamika kwa jina mashuhuri la" Mashati Meusi" kwa kuwa walikuwa wakipendelea kuvaa mavazi meusi. Fikra ya ufashisti iliegemea katika kuasisi utawala wa kidikteta usio wa kibunge na unaopingana na aina yoyote ya uhuru.
Na miaka 458 iliyopita katika siku inayosadifiana na hii ya leo moja kati ya mitetemeko mikubwa ya ardhi duniani ulitokea katika mkoa wa Shaanxi nchini China. Mkoa huo ulikuwa miongoni mwa mikoa ya China yenye watu wengi na kwa msingi huo zilzala hiyo ilisababisha hasara na maafa makubwa kwa wakazi wa eneo hilo. Watu 830,000 wa mkoa wa Shaanxi walipoteza maisha kutokana na mtetemeko huo mkubwa wa ardhi.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi