Siku kama ya leo miaka 1434 iliyopita, ilianza kazi ya
ujenzi wa msikiti wa Mtume mjini Madina ambao ni msikiti wa pili kwa
utukufu duniani baada ya Masjidul Haram. Mtume (SAW) alitoa amri ya
kujengwa msikiti wa Madina baada tu ya kuhamia mjini humo na yeye
mwenyewe alishiriki katika ujenzi wake.Kuta za msikiti huo zilijengwa
kwa kutumia mawe na matofali na paa lake liliezekwa kwa kutumia makuti
ya mitende. Kandokando ya msikiti huo kulijengwa vyumba vya Mtume na
baadhi ya maswahaba zake.
Mtume alitumia msikiti kwa ajili ya masuala mbalimbali ya kiibada, kutoa hukumu baina ya watu, vikao vya mashauriano, mafunzo ya kivita na utatuzi wa masuala mbalimbali ya Waislamu.
Mtume alitumia msikiti kwa ajili ya masuala mbalimbali ya kiibada, kutoa hukumu baina ya watu, vikao vya mashauriano, mafunzo ya kivita na utatuzi wa masuala mbalimbali ya Waislamu.
Mmiaka 114 iliyopita muwafaka na leo alifariki dunia
mwandishi na mshairi maarufu wa Kiingereza John Ruskin. Mshairi huyo
alizaliwa Mwaka 1819 katika familia tajiri na inayoheshimu mafundisho ya
dini. Ruskin alianza kusoma mashairi wakati akiwa bado anasoma. Pia
alikuwa mtaalamu wa masuala ya sanaa na alieleza mitazamo na maoni yake
kuhusu sanaa katika kitabu chake kinachoitwa Modern Painters. Mwandishi
huyu Muingereza alikuwa akiamini kuwa thamani ya sanaa imo katika
kuwasilisha fikra aali kwa walengwa na kwamba sanaa inapaswa kuwa daraja
baina ya dunia hii na ulimwengu wa akhera. John Ruskin anasema katika
kitabu cha The Seven Lamps of Architecture kuwa sanaa ya usanifu majengo
huakisi itikadi za kidini na kimaadili na matakwa ya kitaifa ya watu
husika. Alikuwa na maoni ya kimaadili pia kuhusu masuala ya kiuchumi na
alikuwa na wasiwasi kuhusu mustakbali wa maendeleo na ustawi wa viwanda.
Vitabu vingine vya mwandishi huyo ni "The Stones of Venice", "Unto This Last" na "A Joy Forever".
Vitabu vingine vya mwandishi huyo ni "The Stones of Venice", "Unto This Last" na "A Joy Forever".
Na siku kama ya leo miaka 35 iliyopita ilienea habari ya
kukaribia safari ya Imam Khomeini M.A ya kurejea nchini Iran akitokea
uhamishoni Ufaransa. Habari hiyo ilipokewa kwa shangwe na furaha kati ya
matabaka yote ya wananchi wa Iran. Kwa upande mwingine habari hiyo
ilisababisha wasiwasi na wahaka mkubwa kwa vibaraka wa utawala wa Shah.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!