Home »
siasa afrika
» MAPENDEKEZO YAKUSITISHWA MGOGORA NCHINI SUDAN KUSINI YAWASILISHWA NA WAPATANISHI
MAPENDEKEZO YAKUSITISHWA MGOGORA NCHINI SUDAN KUSINI YAWASILISHWA NA WAPATANISHI
Wapatanishi
katika mgogoro wa Sudani Kusini, wamewasilisha mapendekezo ya kufikia
mkataba wa kusitishwa mapigano kati ya waasi na wanajeshi wa serikali
katika mazungumzo ya huko Addis Ababa nchini Ethiopia, ikiwa ni siku
mbili kabla ya mkutano wa Umoja wa Afrika Kuhusu Sudani Kusini
unatarajiwa kufanyika siku ya Alhaminisi.
Mapendekezo hayo yanawataka waasi kusitisha vita, huku serikali
ikitakiwa kuwaacha huru wafuasi 11 wa makama wa rais wa zamani wa
nchi hiyo Riek Machar wanaoziuliwa katika jela moja mjini Juba.
Kuachiwa huru kwa watu hao 11 ndicho kinakwamisha mazungumzo ya
kusaka amani kati ya pande mbili zinazo gomba chini ya usimamizi wa
jumuiuya ya Igad.Mkutano wa wakuu wa nchi za IGAD unafanyika juma hili mjini Juba
ambapo viongozi wa mataifa hayo wanatarajiwa kusisitiza mazungumzo ya
mjini Addis Ababa kupewa nafasi ili kuzileta pamoja pande mbili
zinazokinzana wakati huu mapigano yakiripotiwa zaidi.Hayo yanajiri wakati rais wa Sudani Omar Hassan Al Bashir akijiandaa
kufanya ziara huko Sudani Kusini ambapo ni miongoni mwa viongozi
wataohudhuria mkutano utaojadili kuhusu Sudani Kusini unaofanyika mjini
Juba alhamisi juma hili.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!