Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » MAUAJI YA WAISLAM NCHINI MYANMAR UINGEREZA INAHUSIKA:BURMA COMPAIGN UK

MAUAJI YA WAISLAM NCHINI MYANMAR UINGEREZA INAHUSIKA:BURMA COMPAIGN UK

Written By Unknown on Monday, 20 January 2014 | Monday, January 20, 2014

Jumuiya ya Kutetea Haki za Binadamu ya Burma Campaign UK imeikosoa serikali ya Uingereza kwa kulisaidia kifedha jeshi la Myanmar linalohusika katika mauaji ya Waislamu nchini humo.
Taarifa ya jumuiya hiyo yenye makao yake mjini London imesema hatua ya serikali ya Uingereza ya kutenga bajeti ya kwa ajili ya kuwapa mafunzo wanajeshi wa Myanmar inasikitisha sana na kuongeza kuwa London inatoa misaada hiyo ya kifedha kwa jeshi la Myanmar bila ya kutoa masharti yoyote ya kuboreshwa haki za binadamu na kufanyika marekebisho ya kisiasa katika nchi hiyo.
Misaada hiyo ya kifedha ya Uingereza kwa Myanmar imetolewa huku ripoti za hivi karibuni zikisema kuwa Mabudha wenye misimamo mikali wa nchi hiyo wakishirikiana na  jeshi la serikali wanaendelea kufanya mauaji dhidi ya Waislamu na kufanya uhalifu kama wa kubaka wanawake Waislamu. Mauaji ya hivi karibuni kabisa ni yale ya mauaji ya makumi ya Waislamu yaliyofanywa  na Mabudha katika mkoa wa Rakhine.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi