Lady Jay Dee aka Anaconda, mwimbaji wa kike ambaye aliumaliza mwaka
jana kwa kuongeza mafanikio makubwa kimuziki kupitia hits zake mbili
zilizogeuka kuwa ‘nyimbo za taifa’, Joto Hasira na Yahaya, mwaka huu atasikika akiwa amezing’arisha ngoma za rappers kadhaa.
Lady Jay Dee amesema kuwa kuna wimbo amefanya na rappers wa Tamaduni Music, Nikki Mbishi, Songa na One The Incredible. Ameongeza kuwa kuna ngoma aliyofanya na mkali wa Bongo Flava Juma Nature, na kwamba anaamini itatoka mapema.
“2014 kuna nyimbo nyingi zitakuja, kuna wimbo nimefanya na One The Incredible utatoka, na kuna wimbo mwingine nimefanya na Juma Nature uko tayari utatoka. Watakapokuwa wao wako tayari kutoa lakini nadhani zitatoka mapema.” amesema.
Amefunguka kuwa mwezi wa Tatu ataachia rasmi official single yake aliyofanya na Bob Junior.
Naye Nikki wa Pili alifunguka kuwa mbali na wimbo wa ‘Kilimanjaro’ wa Joh Makini na G Nako wakiwa na Lady Jay Dee, kuna wimbo mwingine ambao Binti Komando alifanya na Joh Makini ambao bado haujatoka.
Mapema mwaka huu, Jide alionesha gari lake jipya aina ya Range Rover matata ambayo ni moja kati ya matunda ya kazi yake ya muziki.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!