Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch
limeutaka Umoja wa Mataifa kufanya uchunguzi wa kina juu ya vitendo
vya ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na serikali ya Sudan ya
Kusini na waasi nchini humo. Taarifa iliyotolewa jana na shirika hilo la
kutetea haki za binadamu imeeleza kuwa, Umoja wa Mataifa unapasa
kukabiliana kikamilifu na watu wote wanaotuhumiwa kutenda vitendo vya
ukiukaji wa haki za binadamu na haki za mashirika ya kimataifa ya kutoa
misaada nchini humo.
Daniel Bekele Mkurugenzi wa Human Rights Watch katika masuala ya Afrika amesema kuwa, baadhi ya wananchi wa nchi hiyo wamekumbwa na jinai hizo kutokana na masuala ya kikabila. Bekele ameongeza kuwa, shirika hilo lina nyaraka na ushahidi tosha unaoonyesha kwamba, jeshi la Sudan Kusini liliwauwa kwa makusudi watu wa kabila na Nuer mjini Juba.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, mapigano nchini Sudan Kusini yalianza tarehe 15 mwezi ulipita, kati ya vikosi vitiifu kwa serikali ya Rais Salva Kiir, dhidi ya wanamgambo waasi wanaoongozwa na Riek Machar makamu wa zamani wa rais nchini humo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!