Kwa akali watu 74 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa, baada
ya kundi la Boko Haram kufanya mashambulio mawili huko kaskazini
mashariki mwa Nigeria.
Taarifa zinasema kuwa, shambulio la kwanza lilifanyika jana katika soko la kijiji cha Kawuri kilichoko katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki nwa nchi hiyo nakuuawa watu 52 wengine 25 wamejeruhiwa. Jeshi la Polisi limetangaza kuwa, kuna uwezekano mkubwa wa kuongezeka idadi ya wahanga baada ya kuripotiwa kwamba baadhi ya majeruhi wako mahututi. Polisi imeeleza kuwa, shambulio hilo lilifanywa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram waliokuwa wamepanda magari kadhaa. Polisi ya Nigeria imesema, wanamgambo hao walikuwa na mabomu kadhaa ya kienyeji na waliteketeza nyumba na magari kadhaa kabla ya kuondoka kijiji hapo.
Polisi ya Nigeria imetangaza pia kwamba, kundi la Boko Haram limeshambulia Kanisa moja katika jimbo la Adamawa na kuua watu 22. makumi ya wengine pia kujeruhiwa. Harakati za kundi la Boko Haram zimetoa changamoto kubwa kwa serikali ya Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria. Inafaa kuashiria hapa kuwa, serikali ya Abuja imetangaza hali ya hatari katika majimbo matatu ya kaskazini mwa nchi hiyo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!