Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » BAADA YA MUSJID MUSSA YA MOMBASA KUVAMIWA NA MAPOLISI HIVI NDIVYO ZOGO ZILIVYO ANZA KURINDIMA

BAADA YA MUSJID MUSSA YA MOMBASA KUVAMIWA NA MAPOLISI HIVI NDIVYO ZOGO ZILIVYO ANZA KURINDIMA

Written By Unknown on Monday, 3 February 2014 | Monday, February 03, 2014

Vijana walioghadhabishwa na tukio la polisi kuvamia msikiti mmoja unaotumiwa na wahubiri wanaosemekana kuhubiri itikadi kali za kiisilamu mjini Mombasa,Pwani ya Kenya, wamekabiliana na polisi kwa siku ya pili leo.
Duru zinasema kuwa Maafisa wa usalama wanakutana kujadili matukio ya Jumapili mjini Mombasa ambapo polisi waliwakamata vijana katika msikiti wa Musa .

Waliokamatwa walifikishwa mahakamani kujibu makosa ya kujihusisha na ugaidi.
Msako wa polisi ulisababisha vifo vya watu watatu akiwemo polisi mmoja huku wengine wengi wakijeruhiwa.
Polisi walichukua muda wa masaa tatu kuendesha msako, katika msikiti wa Musa mtaani Majengo baada ya kupata habari kuwa mkutano wa vijana kuhusu jihad ulikuwa unaendelea ndani ya msikiti huo.
Zogo lilianza baada ya vijana waliokuwa ndani ya msikiti huo unaohushwa na marehemu Aboud Rogo kuzuia polisi kuingia ndani. Watu watatu waliuawa na wengine kujeruhiwa wakati polisi wakifanikiwa kuwakamata vijana karibu miamoja.
Miongoni mwa waliokamatwa alikuwa mwanawe marehemu Rogo aliyesema kuwa wakati walipokamatwa kulikuwa na bunduki 18 ndani ya msikiti huo na kuwa alihadaiwa kuhudhuria mkutano huo.
Taarifa zinasema kuwa mkutano huo wa vijana uliandaliwa kupitia mitandao ya kijamii huku vijikaratasi vikisambazwa mjini humo kuwaalika watu.

Tazama Picha zaidi za vile ma Polisi walivyo pelekana na waislm huko Mombasa



Polisi na vijana waisilamu wamekabiliana Mombasa baada ya tukio la Jumapili





TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi