Jeshi la Uganda limetangaza kuwa, limeongeza askari 1600 nchini
Somalia kwa ajili ya kuimarisha jitihada za kulinda amani na usalama
katika nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.
Paddy Ankunda, msemaji wa jeshi la Uganda amesema kuwa, askari hao wa kulinda amani wameongezwa kwa lengo la kuimarisha utulivu nchini Somalia hasa katika maeneo ambayo hakuna waasi wa al Shabab.
Askari wa Uganda watapelekewa nchini Somalia chini ya kikosi cha AMISOM na watakuwa katika maeneo ya Banadir, Bas, Markal pamoja na mji mkuu Mogadishu. Uganda ni nchi ya kwanza iliyopeleka wanajeshi wake Somalia mwaka 2007, na hadi sasa inakadiriwa kuwa kuna askari 8,000 wa Uganda nchini humo.

0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!