KIUNGO, Emmanuel Frimpong ametoa kali baada ya kudai uhamisho
wake Barnsley utapunguza kasi ya kuwanasa mademu kwa kuwa klabu hiyo si
maarufu sana.
Staa huyo wa Ghana, aliyeondoka Arsenal kwenye
usajili wa mwezi uliopita alikuwa akiitumia timu hiyo kwa faida ya
kuwanasa mabinti wazuri licha ya kwamba hakuwa akipata namba.
Kwenye kikosi cha Arsenal, Frimpong amecheza mechi
16, huku akiandamwa na majeruhi na kuibuka kwa Jack Wilshere kumemfanya
akose namba klabuni hapo.
Lakini, baada ya kuhama Arsenal na kutimkia
Barnsley, Frimpong aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kwamba
atawezaje kuwapata tena mabinti akiwa na klabu ya daraja la chini.
“Nitawapate mabinti tena,” aliandika Frimpong
kwenye ukurasa wake wa Instagram, lakini ujumbe huo aliufuta haraka
sana. Kwenye kikosi cha Barnsley, Frimpong alianza vibaya baada ya
kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo wake wa kwanza baada ya
kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kumchezea rafu mbili mchezaji mmoja
ndani ya dakika saba.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!