25
Rekodi
ya ushindi mfululizo wakiongoza ligi, iliyowekwa na FC Barcelona
ilifikia tamati baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Valencia na kuporwa
uongozi wa Ligi na Atletico Madrid. Ushindi wa Valencia ulikatiza rekodi
ya kushinda mara 25 mfululizo kwenye la liga zilizochezwa kwenye dimba
la Nou Camp. Valencia imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda
nyumbani kwa Barca tangu Real Madrid walipofanya hivyo mnamo April 2012.
Siku iliyofuatia Atletico Madrid wakashinda 4-0 dhidi ya Real Sociedad,
wakaenda kushika usukani mwa ligi kwa mara ya kwanza tangu waliposhinda
makombe mawili msimu wa 1995/96.
3
Mabao matatu yaliyofungwa na Wesley Sneijder katika
ushindi wa Galatasaray wa 6-0 dhidi ya Bursaspor jumapili iliyopita -
ilikuwa ndio hat trick ya pili ya Sneijder tangu alipoanza kucheza soka
la kulipwa. Pia ilikuwa hat trick ya kwanza katika kipindi cha miaka
saba, mara ya mwisho kufanya hivyo ilikuwa kwenye mchezo wa ushindi wa
4-1 wa Ajax dhidi ya Feyenoord mnamo 4 February 2007. Ushindi huo wa
Gala ulikuwa mkubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni, mara ya mwisho
walishinda ushindi mkubwa ilikuwa walipoifunga Manisaspor 6-3 February
2008.
3
Miaka
mitatu, miezi mitatu ya mechi 61 za matokeo chanya - huo ndio muda
kamili tangu mara ya mwisho Manchester City waliposhindwa kufunga goli
katika mchezo wa ligi kuu ya England uliochezwa nyumbani kwao, lakini
kikosi cha Jose Mourinho kikavunja rekodi hiyo usiku wa Jumatatu, Lakini
pia kikosi cha Jose Mourinho hakikuvunja rekodi hiyo tu bali pia
walivunja rekodi ya City ya kushinda kwenye mechi ya ligi ya nane
mfululizo pia kipigo cha pili katika mechi 22 walizocheza Etihad.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!