Kiwango
cha Luis Suarez msimu kimekuwa katika hali ya juu mno, waandishi kibao
wa habari wamekuwa wakiandika makala za kumsifia huku thamani yake
katika soko la usajili ikipanda maradufu.
Lakini
pamoja na kuwa rekodi nzuri za upachikaji wa mabao msimu huu - ila kuna
kuna sehemu mshambuliaji huyu wa Uruguay anapata zero - hii namba ya
mabao aliyoyafunga dhidi ya vilabu vikubwa kabisa vya ligi kuu ya
England.
Katika
mabao yote 23 aliyoyafunga msimu huu, hakuna hata moja kati ya hayo
lilotinga katika nyavu za vilabu vya Manchester United, Manchester City,
Chelsea au Arsenal – vilabu vilivyoshika nafasi nne za juu msimu
uliopita.
Kiundani zaidi, kati ya mabao hayo ni manne tu amezifunga timu 10 za juu katika msimamo wa ligi.
Je Suarez anavionea vilabu dhaifu tu? Hata ukiangalia rekodi za
REKODI YA UFUNGAJI YA SUAREZ
Timu ambazo Suarez amezifunga msimu huu...
Sunderland (14th kwenye ligi) mabao 2
Crystal Palace (17th) bao 1
West Brom (16th) mabao 3
Fulham (20th) mabao 2
Everton (5th) mabao 2
Norwich (15th)mabao 4
West Ham (18th)mabao 2
Tottenham (6th) mabao 2
Cardiff (19th) mabao2
Hull (13th) bao 1
Stoke (11th)mabao 2
REKODI DHIDI YA TOP 4
(Man Utd, Man City, Chelsea, Arsenal)
2013-14 – 23 goals, 0 against top four. (MECHI 4).
2012-13 – 30 goals, 4 against top four. (Mechi 8).
2011-12 – 17 goals, 2 against top four. (Mechi 8).
2010-11 – 4 goals, 0 against top four. (Mechi 3).
nyuma ya msimu huu, takwimu zinaonyesha hivyo.
Ni
mara 74 mshambuliaji huyo wa Uruguay ameweza kubusu mishipa ya kiganja
chake akishangilia mabao anayoyafunga tangu ajiunge na Liverpool, lakini
mabao 6 tu kati ya hayo amezifunga timu za TOP 4, na hayo yamepatikana
baada ya mechi 23.
Wakati
huo huo, amefunga mabao 11 dhidi ya timu ya Norwich. Pia katika miaka
yote hii ameifunga Manchester United goli moja tu miaka miwili iliyopita
katika dimba la Old Trafford.
Msimu
huu, Suarez alifunga mabao 10 katika mechi nne tu mapema mwezi Desemba
kabla ya Liverpool haijangia katika wakati muafaka wa kuamua hatma yao
ya ubingwa msimu huu waliposafiri kwenda kucheza na Manchester City na
Chelsea, katika michezo hiyo muhimu, Suarez alitoka kapa, huku Liverpool
akifungwa mechi zote - pia alishindwa kufanya chochote katika mchezo
dhidi ya Arsenal na hata dhidi ya Manchester United katika kombe la ligi
- pia mechi hizo zote Liverpool walifungwa.
Jumamosi
hii, wanakutana na viongozi wa ligi Arsenal katika dimba la Anfield.
Ndio kwa ukali wa Suarez kuzifumania nyavu dhidi ya timu za chini umeipa
nafasi Liverpool ya kuweza kusogolea Top 3.
Ingawa
kwa hilo ili liweze kutokea inabidi Liverpool ianze kushinda dhidi ya
vilabu hivyo vikubwa, mabao na uchezaji mzuri wa Suarez unahitajika
kufanikisha hilo.
Wapinzani
wao wa Jumamosi, Arsenal, ndio timu ile ile iliyojaribu kumnyakua
Suarez kutoka Merseyside kwenda London ya kaskazini wakati kiangazi
walipotuma ofa ya £40m-plus-£1.
Kwa
kuwa na Suarez, iliaminika wangeweza kushindania ubingwa, lakini hata
baada ya kumkosa wanaonekana kuwa vizuri mno katika harakati zao za
kumaliza ukame wa miaka 9 bila kombe.
Arsenal nao, wameshindwa kufnya vizuri dhidi ya kubwa kama United, City na Chelsea, kama ilivyo kwa Suarez.
Wikiendi
hii Suarez ana nafasi ya kuwafunga midomo wachambuzi wa soka walio na
mashaka juu ya uwezo wake dhidi ya vilabu vikubwa na kuiwezesha timu
yake kuisogelea top 3 ya EPL. Je ataweza kuisimamisha Arsenal iliyo on
fire???? Muda utatoa majibu.
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!