Headlines News :
USWAZI MAGAZINE
Home » » SERIKALI ZA UINGEREZA NA UFARANSA ZAIJIA JUU KWA JUU SERIKALI YA SYRIA KWA SHUTMA ZAKUZOROTESHA MAZUNGUMZO YA AMANI YA GENEVA

SERIKALI ZA UINGEREZA NA UFARANSA ZAIJIA JUU KWA JUU SERIKALI YA SYRIA KWA SHUTMA ZAKUZOROTESHA MAZUNGUMZO YA AMANI YA GENEVA

Written By Unknown on Sunday, 16 February 2014 | Sunday, February 16, 2014

Uingereza na Ufaransa zimeilaumu serikali ya Syria kwa kuzorotesha mazungumzo ya amani kati yao na upinzani huko Geneva.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza William Hague amesema lawama zote zinapaswa kuelekezwa kwa utawala wa Assad huku waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Laurent Fabius akisema serikali hiyo imezuia ufanisi wa mazungumzo hayo.
Hali hiyo ilimsukuma Mpatanishi wa mzozo wa syria Lakhdar Brahimi kutaka radhi raia wa Syria kufuatia kumalizika kwa mazungumzo ya Geneva bila kuwa na matumaini ya kutatuliwa kwa mzozo huo.
Kiongozi huyo alikutana katika majadiliano ya mwisho na pande mbili huko geneva kumaliza mzozo uliopo kati ya serikali ya Syria na upinzani nchini humo ambapo hoja ya msingi ilikuwa ni hatua ya serikali kukataa kuzungumzia utawala wa mpito.
Hata hivyo pande zote mbili zimekubaliana juu ya ajenda za kujadiliwa katika mzunguko wa pili, ambapo Brahimi alisema serikali ya Syria ilikataa maoni yake yaliyotaka kuanzwa kwa mazungumzo ya awamu ya tatu katika mjadala utakaolenga kupambana na ukatili, ugaidi, na baadaye kujadili serikali ya mpito.
Mzozo nchini Syria umegharimu maisha ya watu zaidi ya laki moja tangu ulipozuka mwaka 2011 mnamo mwezi March.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
Share Na Jamaa Yako :

0 comments:

Toa Maoni yako

Tuambie Unafikilia Nini..!

Followers

Facebook Fan Page

Tukutane Twitter

Walio Tembelea Website Hii

Advertise

Smiley face
 
Support : Ismail Niyonkuru | Gody Godwin Unstoppable
Proudly powered by Blogger
Copyright © 2011. Ahabona 24 - Haki Zote Zimehifadhiwa
Template Design by Gody Godwin Unstoppable Published by Uswazi