Beki
wa klabu ya Arsenal Per Mertesacker amefunguka na kusema wale watu wote
waliokuwa na mashaka juu ya uwezo wake pamoja na beki mwenza wa kati wa
Gunners hawakuwa sahihi baada ya ushirikiano wake na Laurent Koscienly
kutimiza miaka miwili bila kufungwa katika premier league kila
wanapocheza pamoja.
Ushirikiano
wa mabeki hao wawili wa kati sasa umetimiza jumla ya mechi 32 za
premier league bila kufungwa kila wanapocheza pamoja.
Rekodi
zinaonyesha tangu walipofungwa 2-1 na Manchester United katika dimba la
Emirates January 22, 2012, wawili hao hawajapoteza mechi yoyote
waliyocheza pamoja.
Hata
hivyo, takwimu zinaonyesha kwamba rekodi yao ilitiwa doa katika mchezo
dhidi ya Manchester City waliofungwa 6-3 - lakini hawakucheza pamoja
kwa dakika zote tisini, Koscielny alitolewa nje kabla ya mapumziko, pia
katika mchezo dhidi ya Aston Villa ambao pia walifungwa 3-1, beki wa
kifaransa alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya dakika 25 za mchezo.
TOA MAONI YAKO HAPA CHINI
0 comments:
Toa Maoni yako
Tuambie Unafikilia Nini..!